• 7:24 AM
  • Mbeya Info
  • Fursa na Masoko, Mafunzo kwa Video, Wajasiriamali

ufugaji wa samaki

Tujifunze kuhusu ufugaji wa samaki wa kisasa ambao
hufanyika kwenye mabwawa ya kuchimbwa au visima
na vitu vingine vinavofanana na hivyo.
Kuna aina nyingi za samaki wa maji baridi ambao
wanaweza kufugika kwa urahisi au ugumu kidogo tu
na aina hizo wapo wale ambao sio wa kuzaliana
(monosexual) na wale wa kuzaliana(heterosexual)
Urahisi hapa uko zaidi kwenye kuwafuga wasiozaliana
sababu hawaongezeki wakati wale wanaozaliana
utakuwa na utaratibu wa kuhamisha fishling
(vifaranga) sehemu nyingine.
Rasilimali muhimu za kuwa nazo ili kufanikisha
shughuli hii ni eneo la ardhi,maji, rasilimali watu na
rasilimali fedha.Eneo la ardhi ndio litakaloonyesha ni
kwa namna gani bwawa lako liwe,aidha la kujengea
na cement,kutandika plastic au kuchimba na
kulitumia hivyohivyo.Bwawa huchimbwa/kujengwa
kwa kuwa na sakafu yenye ulalo kiasi(gentle slope/
gradient)
Wapo samaki aina ya Sato(Tilapia),Kambale(African
catfish) na wengine aina ya pangasius ambao
hufugwa kwa wingi sana.
Unahitaji samaki 7-8 katika meter moja ya mraba
(1m^2) ,kwa maana hiyo kama una meter za mraba
600 nasi unaweza kufuga samaki 4500.Haishauriwi
kulundika samaki kwenye eneo dogo kwani
itawasababishia ukosefu wa hewa(oxygen).Ingawa
zipo njia za kuweza kuongeza upatikanaji wa hewa
kwenye mabwawa.
Ukishachimba bwawa lako(aidha na kulijengea)
unaingiza maji kwenye bwawa hakikisha yamekaribia
futi 2.5 mpaka kujaa full.Itakubidi kufanya liming
(kumwagia chokaa bwawa kabla ya kuweka maji ili
kuua bacteria hatarishi kwa maisha na afya ya
samaki wako) pia unahitajika kuyarutubisha hayo maji
kwa kuchanganya na mbolea(kama ya ng'ombe na za
viwandani pia ingawa haishauriwi sana) na kusubiria
kwa muda usiopungua siku 21 au zaidi.Unafanya hivi
ili kuweka mazingira ya chakula asili(natural foood)
kwa ajili ya samaki kujitengeneza,vyakula hivo hua
katika hali ya mimea na viumbe wadogo
(microorganisms)
Upatikanaji wa vifaranga vya samaki,hapa inakubidi
uwe makini sana kama umeamua kuzalisha
sato,changamoto kubwa ya sato ni kupata mbegu
ambayo under right conditions vifaranga vitaweza kua
samaki wenye uzito wa kutosha(miezi 6 awe at least
500grams au zaidi).Mbegu ya sato hupatikana kwa
bei rejareja ya sh 300 na kambale sh 500 kwa
kifaranga kimoja.Wapo wazalishaji wengi wa mbegu
za vifaranga wa ndani na nje ya nchi ila kwa
Tanzania nimewakubali Tanzania Fisheries Research
Institute(TAFIRI) Nyegezi,Mwanza(Nimefwatilia
performance yao shambani).
Ulishaji wa vifaranga vyako ,chakula chao
kinategemea na uzito wao mfano samaki hula 5% ya
uzito wake wa mwili akiwa mdogo na 3% akiwa
mkubwa.Hapa tunaongelea ulishaji wa chakula cha
ziada(supplement food),sababu cha asili amekipata
kwenye ile mbolea ulioweka.Kama una vifaranga 100
vyenye gram 10 kila kimoja basi utahitaji gram 50
kuwalisha.
Itakuchukua Miezi 6-9 kuanza kuvuna samaki wako
ambao unaweza kuwauza kulingana na uzito au au
njia utayoona inakufaa.Samaki wengi wa kwenye
mabwawa wanavunwa kwa kutumia nyavu au
kumwaga maji yote nje ya bwawa.Masoko yake haya
samaki ni pamoja na supermarkets, wafanyabiashara
sokoni na mitaani pamoja na watu binafsi.
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Older Post → Home

Copyright © Mjasiriamali | Powered by Blogger