• 7:24 AM
  • Mbeya Info
  • Fursa na Masoko, Mafunzo kwa Video, Wajasiriamali

ufugaji wa samaki

Tujifunze kuhusu ufugaji wa samaki wa kisasa ambao
hufanyika kwenye mabwawa ya kuchimbwa au visima
na vitu vingine vinavofanana na hivyo.
Kuna aina nyingi za samaki wa maji baridi ambao
wanaweza kufugika kwa urahisi au ugumu kidogo tu
na aina hizo wapo wale ambao sio wa kuzaliana
(monosexual) na wale wa kuzaliana(heterosexual)
Urahisi hapa uko zaidi kwenye kuwafuga wasiozaliana
sababu hawaongezeki wakati wale wanaozaliana
utakuwa na utaratibu wa kuhamisha fishling
(vifaranga) sehemu nyingine.
Rasilimali muhimu za kuwa nazo ili kufanikisha
shughuli hii ni eneo la ardhi,maji, rasilimali watu na
rasilimali fedha.Eneo la ardhi ndio litakaloonyesha ni
kwa namna gani bwawa lako liwe,aidha la kujengea
na cement,kutandika plastic au kuchimba na
kulitumia hivyohivyo.Bwawa huchimbwa/kujengwa
kwa kuwa na sakafu yenye ulalo kiasi(gentle slope/
gradient)
Wapo samaki aina ya Sato(Tilapia),Kambale(African
catfish) na wengine aina ya pangasius ambao
hufugwa kwa wingi sana.
Unahitaji samaki 7-8 katika meter moja ya mraba
(1m^2) ,kwa maana hiyo kama una meter za mraba
600 nasi unaweza kufuga samaki 4500.Haishauriwi
kulundika samaki kwenye eneo dogo kwani
itawasababishia ukosefu wa hewa(oxygen).Ingawa
zipo njia za kuweza kuongeza upatikanaji wa hewa
kwenye mabwawa.
Ukishachimba bwawa lako(aidha na kulijengea)
unaingiza maji kwenye bwawa hakikisha yamekaribia
futi 2.5 mpaka kujaa full.Itakubidi kufanya liming
(kumwagia chokaa bwawa kabla ya kuweka maji ili
kuua bacteria hatarishi kwa maisha na afya ya
samaki wako) pia unahitajika kuyarutubisha hayo maji
kwa kuchanganya na mbolea(kama ya ng'ombe na za
viwandani pia ingawa haishauriwi sana) na kusubiria
kwa muda usiopungua siku 21 au zaidi.Unafanya hivi
ili kuweka mazingira ya chakula asili(natural foood)
kwa ajili ya samaki kujitengeneza,vyakula hivo hua
katika hali ya mimea na viumbe wadogo
(microorganisms)
Upatikanaji wa vifaranga vya samaki,hapa inakubidi
uwe makini sana kama umeamua kuzalisha
sato,changamoto kubwa ya sato ni kupata mbegu
ambayo under right conditions vifaranga vitaweza kua
samaki wenye uzito wa kutosha(miezi 6 awe at least
500grams au zaidi).Mbegu ya sato hupatikana kwa
bei rejareja ya sh 300 na kambale sh 500 kwa
kifaranga kimoja.Wapo wazalishaji wengi wa mbegu
za vifaranga wa ndani na nje ya nchi ila kwa
Tanzania nimewakubali Tanzania Fisheries Research
Institute(TAFIRI) Nyegezi,Mwanza(Nimefwatilia
performance yao shambani).
Ulishaji wa vifaranga vyako ,chakula chao
kinategemea na uzito wao mfano samaki hula 5% ya
uzito wake wa mwili akiwa mdogo na 3% akiwa
mkubwa.Hapa tunaongelea ulishaji wa chakula cha
ziada(supplement food),sababu cha asili amekipata
kwenye ile mbolea ulioweka.Kama una vifaranga 100
vyenye gram 10 kila kimoja basi utahitaji gram 50
kuwalisha.
Itakuchukua Miezi 6-9 kuanza kuvuna samaki wako
ambao unaweza kuwauza kulingana na uzito au au
njia utayoona inakufaa.Samaki wengi wa kwenye
mabwawa wanavunwa kwa kutumia nyavu au
kumwaga maji yote nje ya bwawa.Masoko yake haya
samaki ni pamoja na supermarkets, wafanyabiashara
sokoni na mitaani pamoja na watu binafsi.
Read More
  • 7:22 AM
  • Mbeya Info

kilimo cha ufuta

KILIMO BORA CHA UFUTA
Ufuta (sesamum indicum)ni zao linalolimwa kwa
wingi katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani,
Morogoro, Dodoma, Tanga na ukanda wa chini katika
mikoa ya Rukwa na Mbeya. Zao hili hulimwa kwa ajili
ya chakula na biashara. Mbegu za zao hili huwa na
wastani wa mafuta kiasi cha asilimia 45.
MAMBO YA KUZINGATIA WA KATI WA KUZALISHA
MBEGU
• Chagua aina ya mbegu inayotoa mazao mengi na
bora, inayovumilia mashambulizi ya magonjwa na
wadudu, inayokomaa mapema na kutoa mafuta
mengi.
• Chagua mbegu inayokomaa kwa pamoja ili
kurahisisha uvunaji na pia kuepuka upotevu wa zao
shambani.
• Aina nyeupe ya mbegu ya ufuta hupendelewa zaidi
kuliko aina nyeusi.
MBOLEA
Ufuta unahitaji rutuba ya kutosha ili kutoa mazao
bora. Katika kudumisha rutuba ya udongo, tumia
kilimo cha mzunguko wa mazao au weka mbolea za
asili pale inapobidi.
PALIZI
Dhibiti magugu kwa kupalilia ili kuruhusu ufuta
kutumia vizuri unyevu na virutubishi. Magugu mengine
huwa ni maficho ya wadudu waharibifu wa zao la
ufuta.
MAGONJWA NA WADUDU
Ufuta hushambuliwa na magonjwa na wadudu
mbalimbali ambao huweza kusababisha upungufu na
ubora wa mazao. Hivyo kagua shamba mara kwa
mara hasa kwenye maua na mapodo ili kuona dalili za
mashambulizi. Endapo kuna dalili zamashambulizi,
chukua tahadhari mapema kabla ya uharibifu mkubwa
haujatokea.
MAANDALIZI KABLA YA KUVUNAKAGUA SHAMBA
• Kagua shamba kuona kama ufuta umekomaa.
• Ufuta hukomaa, kati ya miezi mitatu na minne tangu
kupanda kutegemea aina.
• Aina ya ufuta usiokuwa na matawi hukomaa
mapema kuliko ile yenye matawi.
• Ni muhimu kuwahi kuvuna ili kuepuka ufuta
kupukutikia shambani.
DALILI ZA KUKOMAA UFUTA SHAMBANI
• Kwa kawaida majani hubadilika rangi kutoka kijani
na kuwa ya manjano na hatimaye kudondoka.
• Mashina hubadilika rangi kutoka kijani na kuwa ya
kahawia.
VIFAA VYA KUVUNIA
• Kamba
• Siko
• Panga
VIFAA VYA KUKAUSHIA
• Sehemu ya kukaushia yenye Sakafu ya saruji
• Maturubai
• Sakafu safi
USAFIRI
• Mikokoteni
• Matela ya matrekta
• Magari
KUVUNA
• Vuna ufuta mapema kabla mapodo kukomaa sana
na kuanza kupasuka na kuachia punje.Mapodo ya
ufuta yaliyokomaa sana yakiguswa au kutikiswa na
upepo hupasuka na kuachia mbegu, hali
inayosababisha upotevu mkubwa.
• Mbegu za ufuta ni ndogo na zikidondoka chini ni
vigumu kuziokota. Vilevile mbegu zilizodondoka ni
vigumu kuzitenganisha na uchafu.
• Uvunaji wa ufuta huhusisha ukataji wa mimea yenye
mapodo kwa kutumia vyombo vya mkono kama panga
kwa kukata mashina.
• Kwa aina za ufuta zenye mapodo yanayopasuka,
uvunaji ufanyike wakati mimea bado ni kijani ili
kuepuka upotevu wa mbegu.
• Aidha uvunaji ufanyike wakati hakuna upepo wala
jua kali.
• Baada ya kukata mashina yafunge katika mizigo
midogo na kuweka katika vyombo vya kusafirisha
kama vile mikokoteni, matela au magari hadi sehemu
ya kukaushia.
• Panga mizigo midogo kwa kusimamisha katika
malundo madogo yasiyozidi mizigo minane kwenye
sehemu safi za kukaushia.
KUKAUSHA
Mapodo ya ufuta hukaushwa yakiwa yamefungwa
katika vitita. Vitita huwekwa kwa kuegeshwa kwenye
fremu ya kukaushia kwa muda wa wiki mbili hadi tatu
kutegemea hali ya hewa. Fremu hii huwekwa juu ya
turubai au sakafu ili kuzuia upotevu wa punje
kutokana na kupasuka kwa mapodo.
KUPURA
Upuraji hufanyika kwenye turubai, mkeka au kwenye
sakafu safi.
• Vitita hupigwa taratibu kwa kutumia mti au
hutikiswa vikiwa vimegeuzwa vichwa chini ili
kuruhusu punje za ufuta kudondoka kwenye sakafu
safi au turubai.
KUPEPETA NA KUPEMBUA
Kupepeta na kupembua hufanywa ili kuondoa
takataka kama vile mawe, vipande vya mapodo,vijiti
na vumbi.Njia bora ya kupepeta na kupembua ni kwa
kutumia mikono.
• Ufuta huwekwa kwenye vyombo kama vile ungo kwa
kiasi cha kilo mbili hadi tatu. Ufuta hurushwa hewani
kwa kasi ndogo na takataka nyepesi huchukuliwa na
upepo. Zile nzito huondolewa kwa mikono.
KUFUNGASHA
Mbegu za ufuta zilizo safi huwekwa kwenye
vifungashio kama vile magunia madogo ya aina ya
juti ya ujazo wa kilo 50.
• Fungasha mbegu za ufuta kwenye magunia yenye
uzito usiozidi kilo 50. Kabla ya kufungasha hakikisha
mbegu zimekauka hadi kufikia unyevu wa asilimia 10.
KUHIFADHI
• Panga magunia ya ufuta juu ya chaga.
• Panga kwa kupishanisha ili kuruhusu mzunguko wa
hewa kati ya magunia.
KUSINDIKA MBEGU ZA UFUTA
Ufuta husindikwa kupata bidhaa ya mafuta ambayo
hutumika katika mapishi mbalimbali. Mafuta
hukamuliwa kwa kutumia njia za asili na kwa kutumia
mashine. Njia za asili zina ufanisi mdogo
ukilinganisha na zile za kukamua kwa mashine, hivyo
ni vyema kutumia mashine. Kuna mashine za aina
mbili zinazotumika kukamua mafuta; mashine za
mkono na zile zinazoendeshwa kwa injini au mota ya
umeme. Mashine za mikono zinazotumika zaidi hapa
nchini ni za aina ya daraja (Bridge press) na Ram.
KUKAMUA KWA MASHINE YA DARAJA
Mashine ya daraja ni moja ya mashine za kisasa
zinazoweza kukamua mafuta ya ufuta. Mashine hizi
huendeshwa kwa mikono na zina uwezo wa kukamua
mafuta kwa asilimia 68 hadi 72. Inaweza kukamua
kilo 25 za ufuta kwa saa moja. Ili kupata ufanisi
mzuri wa mashine hii, ni muhimu ufuta uwe na
unyevu wa kati ya asilimia 11 na 13. Iwapo unyevu
utakuwa chini ya kiwango hicho inashauriwa
kunyunyizi maji kwenye ufuta kabla ya kukamua.
VIFAA VYA KUKAMULIA MAFUTA
• Mashine ya daraja
• Sufuria • Vifungashio
• Mifuko midogo ya nguo au viroba vyenye upana wa
sentimita 20 na urefu wa sentimita 20.
• Chombo cha kukinga mafuta.
• Chujio safi
• Lebo
• Lakiri Malighafi
• Mbegu za ufuta safi
• Maji safi
UKAMUAJI MAFUTA
• Nyunyuzia maji kidogo kwenye ufuta ili kuongeza
unyevu kufikia asilimia 11 hadi 13. Mafuta hutoka
vizuri kwenye kiwango hicho cha unyevu.
• Jaza ufuta kwenye vifuko vya nguo au viroba
• Vipange vifuko hivyo kwenye silinda na kuanza
kuzungusha mhimili hadi mafuta yaanze kutoka
kupitia matundu ya silinda.
• Acha kwa muda mafuta yaendelee kutoka kisha
endelea kuzungusha mhimili hadi mafuta yaishe.
Mhimili ukiacha kuzunguka ni dalili kuwa mafuta
yamekwisha.
• Kusanya mafuta, chuja na fungasha kwenye chupa
safi zilizochemshwa. Hakikisha chupa ni kavu na zina
mifuniko.
• Weka lebo na lakiri
• Hifadhi mahali pakavu na pasipo na mwanga mkali.
MASHINE YA RAM
Mashine ya Ram ina uwezo wa kusindika kilo 7 za
mbegu za ufuta kwa ufanisi wa asilimia 57%.Aina ya
Ram (BP-30) ina uwezo wa kukamua lita 20 za
mafuta kwa siku.
VIFAA
• Ndoo
• Mashine ya Ram
• Kichujio au kitmbaa safi
• Vifungashio safi
UKAMUAJI
• Anika mbegu za ufuta juani kwa kuzitandaza
kwenye mabati ili zipate joto la kutosha.
• Lengo la kuanika mbegu juani ni kurahisisha
ukamuaji wa mafuta.
• Jaza mbegu za ufuta kwenye mpare wa kulishia
• Funga wenzozuia (HANDLE)ili mbegu za ufuta
zisitoke.
• Nyanyua wenzozuia mpaka juu ili kuruhusu mbegu
za ufuta kuingia kwenye silinda.
• Shusha wenzozuia chini ili kuruhusu pistoni
kusukuma mbegu za ufuta ziingie ndani ya eneo la
shindilio
. • Nyanyua tena wenzozuia mpaka juu na kushusha
na wakati huohuo ukiendelea kujaza mbegu za ufuta
kwenye mpare wa kulishia. Wenzoinua ukiwa mzito ni
dalili kuwa msukumo wa kutosha umejengeka.
Msukumo huo utasababisha mafuta kutoka.
• Mafuta yanapoanza kutoka legeza wenzozuia ili
kuruhusu mashudu kutoka.
• Chuja na hifadhi mafuta kwenye vyombo safi vyenye
mifuniko vilivyochemshwa.
MATUMIZI
Mafuta ya ufuta hutumika katika mapishi mbalimbali
ili kuongeza ladha. Pia husaidia kuleta nguvu na joto
mwilini. Mbegu za ufuta huchanganywa na vyakula
mbali mbali kama mikate, keki, mboga na kadhalika.
Kwa hisani ya mdau MITIKI -KILIMO KWANZA:
KILIMO BORA CHA UFUTA
By frankclemence:
UFUTA
Ni zao linalostahimili baridi na hulimwa maeneo
yasiyozidi mita 1500 juu ya usawa wa bahari.Mvua ni
Kati ya milimita 400-500 ambazo hutosha kabisa kutoa
mavuno Mengi.
AINA ZA MBEGU
Ziada 94,inakomaa Kwa siku 120-130 na inastahimili
magonjwa.Ina uwezo wa kutoa mavuno zaidi ya kilo
1000 Kwa heka.
Nal 92,inakomaa Kwa siku 90-110 na inastahimili
magonjwa hasa mabaka ya majani.Ina uwezo wa kutoa
mavuno kiasi cha kilo 1200-1500 Kwa heka.
MAGONJWA NA NAMNA YA KUYAZUIA
Magonjwa makubwa ya UFUTA ni mabaka na ukungu
kwenye majani.Magonjwa haya yasipozuiwa
yatapukutisha majani na hivyo kusababisha Mazao
kupungua.
KIZUIA
Panda UFUTA mapema
Tumia mboga zinazostahimili magonjwa Kama-Nal
92
Ng'o mimea iliyoathirika
Tumia kilimo cha mzunguko
Read More
  • 7:20 AM
  • Mbeya Info

kilimo cha matikiti

Kilimo cha Matikiti Maji


Mahitaji
1. Shamba la eka 5
2. Mbegu
3. Gharama za uendeshaji wa shamba

Matikiti maji aina ya Sugar baby yanachukua siku 60 toka kupandwa hadi kuvuna na kwa mwaka unaweza kulima mara 4 .

Upandaji:
Nafasi ya shimbo moja kwenda lingine  ni 2mx2m na kila shimo unatakiwa kuweka  mbegu 2 ambazo zinazaa matunda 2 - 3  ambayo wakati wa mavuno hukupatia matunda 4 - 6

Hivyo kwa spacing hiyo napata mashimo 1000-1200

Idadi ya matunda
Mashimo x Matunda kwa shimo x ekari 1,000 x 5 x 5 = 25,000

Mapato
Wastani wa shilingi 500 kwa tikiti x idadi ya matikiti kwa eneo la ekari 5 25,000 x 500 = 12,500,000

Mapato kwa mwaka
12,500,000 x 4 = 50,000,000


Gharama za uendeshaji wa shamba kwa mwaka ni Tsh 25,000,000
Read More
  • 7:18 AM
  • Mbeya Info

Ufugaji wa nyuki

 Tanzania ina mazingira mazuri ya kuzalisha mazao ya nyuki kwa kuwa kuna mimea mingi ambayo inatoa maua yenye kutoa mbochi na chavua vitu ambavyo huwavutia nyuki na kutengeneza asali

Katika Tanzania mazao makuu yatokanayo na ufugaji wa nyuki ni asali na nta. Hata hivyo kuna mazao mengiambayo yanaweza kuzalishwa kutokana na asali na nta.

Tanzania tumejaliwa maeneo mengi sana na makubwa yenye misitu minene yenye chavua na nectar kwa wingi,maeneo hayo yapo karibu Tanzania nzima hayana matumizi yoyote yale ya ufugaji wa nyuki, kwa nchi nyingi Afrika kama vile Ethiopia na nchi nyinginezo ambazo zinasemekana kuongoza kwa ufugaji nyuki zinatamani sana maeneo mazuri tuliyonayo.

Maisha ya Nyuki


 Nyuki ni mdudu mwenye mabawa manne angavu na mwiba nyuma ya mwili wake anayekusanya mbewele ya maua kama chakula chake. Aina inayojulikana hasa ni nyuki wa asali wa familia apis. Kuna spishi zaidi ya 20,000 zinazojumlishwa na biolojia kati ya nyuki lakini wale wa jenasi apis wanaokusanya asali inayovunwa na wanadamu.

Nyuki za asali mara nyingi wanafugwa lakini wengine wanaishi porini na asali yaoinakusanywa kwa kuvunja mzinga wao. Katika Afrika kwa jumla sehemu ya asali bado inatokana na nyuki wa porini lakiniufugaji nyuki unapanuka

Hapo Mwanza wanajamii walikuwa wanafuga nyuki kwenye magome ya miti, vibuyu, vyungu, mapango, vichuguuna kwenye miamba. Baada ya muda ufugaji ulipiga hatua kidogo na watu wengi wakawa wanafuga kwa kutumia mizingailiyochongwa kutoka kwenye magogo ya miti. Ufugaji wa aina hii umedumu kwa karne nyingi kote nchini Tanzania



 Kutokana na uhitaji na ongezeko la matumizi ya bidhaa za nyuki, kulifanyika tafiti mbalimbali ambazo ziliweza kuboresha ufugajiwa nyuki kwa kuwa na mizinga ya kisasa ambayo imewezesha uzalishaji wa asali kuwa mkubwa na kuongeza pato la wafugaji tofautina ilivyokuwa hapo awali. Tafiti hazikuishia kwenye kuboresha mizinga tu, ila siku hadi siku kunavumbuliwanamna bora zaidi za kuimarisja uzalishaji wa nyuki

Hii ni aina mpya ya ufugaji wa nyuki ambao unaweza kujenga kibanda au nyumba kisha kuweka mizinga idadi unayohitaji.

Ni kwa nini kujenga nyumba au kibanda?

Ni muhimu kufuga nyuki kwenye kibanda au kwenye nyumba kwa sababu inasaidia kudhibiti wizi wa mizinga, pamoja na wanyamawanaokula asali na kudhuru nyuki
Inarahisisha utunzaji wa mizinga na kuwafanya nyuki wasihame kwenda sehemu nyingine
Inasaidia watu wengi kujifunza namna nzuri ya ufugaji wa nyuki, ikiwa ni pamoja na watoto, jambo ambalo linafanyashughuli hii kuwa endelevu
Ufugaji wa aina hii unasaidia kuwakinga nyuki dhidi ya majanga kama vile moto, na mafuriko.
Inawaepusha nyuki na usumbufu unaoweza kuwafanya wasizalishe kwa kiwango kinachotakiwa
Uzalishaji unaongezeka. Hii ni kwa sababu mizinga inayotumika ni ile ya kibiashara. Mzinga 1 unapata asali kilo 30 sawa na lita 20

AINA YA NYUMBA


Unaweza kujenga nyumba yenye upana wa futi 3 na urefu wa futi 9. Nyumba hii inaweza kuchukua mizinga hamsini. Halikadhalka, unaweza kujenga kibanda chenye ukubwa sawa na huo
Read More
  • 7:18 AM
  • Mbeya Info

JIFUNZE KILIMO CHA MAPAPAI, FURSA INAYOWEZA KUKUTOA

Papai ni tunda lenye ladha nzuri, na rahisi kuliwa. Aina hii ya tunda ni chanzo cha virutubisho muhimu mwilini, ambavyo husaidia kujenga mwili.



Zao hili asili yake ni ukanda wa kitropiki ambao hauna baridi kali na joto kiasi.



Udongo



pawpaw 2Mipapai hustawi vizuri kwenye udongo usiotuhamisha maji. Endapo maji yakituama kwenye eneo lililopandwa mipapai kwa muda wa siku mbili, mpapai unaweza kuoza kwa haraka na kufa. Kwa kuwa mipapai haina mzizi mkuu, inahitaji udongo wenye rutuba ya kutosha. Halikadhalika, zao hili halihitaji udongo wenye kina kirefu, hivyo ni muhimu kumwagilia mipapai wakati wa kiangazi. Wakati wa mapapai kuiva kama kuna ukame basi hali hiyo huongeza ubora wa papai ikiwamo kutooza mapema baada ya kuvunwa.



Kupanda



Mipapai ipandwe sehemu ambazo hazina upepo mkali. Hii itasaidia mipapai kukua vizuri bila kuvunjika kwani mti wa mpapai huvunjika kirahisi. Inashauriwa kupanda miti ya kukinga upepo kuzunguka shamba la mipapai. Ili kuwa na tija zaidi, unaweza kupanda aina nyingine ya miti ya matunda kama vile miparachichi, na miembe.



Hakikisha miti ya kukinga upepo inakuwa mirefu kuzidi mipapai. Miti hiyo inaweza kutangulia kupandwa miezi kadhaa kabla ya kupanda mipapai.



Mbegu



Kusanya mbegu toka kwenye mapapai makubwa na yaliyo komaa na kuiva, kisha kausha mbegu vizuri kabla ya kupanda. Inashauriwa kununua mbegu kutoka kwa wazalishaji wanaoaminika na waliothibitishwa, ili kuwa na mazao bora zaidi na yanayoweza kukabiliana na magonjwa.



Mbegu aina ya red royal F1, inasifika zaidi kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kukabiliana na magonjwa yanayoshambulia mipapai, na huanza kuvunwa mapema zaidi, kati ya miezi 6 hadi 12. Aina hii huvunwa mfululizo kwa miaka 5 hadi 7.



Uandaaji wa shamba



Inashauriwa kuandaa shamba vizuri kwa kuondoa visiki na magugu yote. Shamba lilimwe vizuri, na kuhakikisha udongo umelainika vizuri.



Mashimo



• Chimba shimo kwa ajili ya kupanda mpapai, liwe na kina cha sentimita 60 na upana wa sentimita 60.

• Weka mboji debe moja kisha changanya na nusu ya udongo uliotoa kwenye shimo, kisha rudishia kwenye shimo.

• Mwagilia maji kwa kipindi cha wiki mbili kabla ya kuotesha.



Kuotesha



Sia miche kwenye kitalu, kasha hamishia shambani inapokuwa na urefu wa sentimita 30. Chomeka mche kwenye ardhi kina cha kati ya sentimeta 1 – 2 chini ya udongo kwenye shimo uliloandaa. Hii itasaidia mche kupata joto la wastani na kuepuka mche kuoza na kufa. Baadhi ya wakulima hupenda kuotesha mipapai moja kwa moja shambani.



Endapo unapenda kufanya hivyo, zingatia haya;



• Kabla ya kupanda mbegu weka mchanganyiko wa majivu na mbolea ya kuku au mboji sehemu unayokusudia kupanda. Mbolea husaidia ukuaji haraka na jivu husaidia kukinga mipapai na magonjwa.

• Panda mbegu 3 – 4 kila shimo, hii ni kwa sababu miche mingine inaweza kufa kutokana na magonjwa, kuliwa na wadudu au ikaota mipapai dume.



Nafasi



Shimo hadi shimo, liwe na nafasi ya mita 3, na mstari hadi mstari mita 3. Hii itasaidia miche ya mipapai kukua vizuri bila kusongamana.



Punguza miche



Baada ya miezi 3 – 5 tangu kupanda, mipapai itaanza kutoa maua na hapo jinsia ya mipapai itajulikana. Inapofikia wakati huo inabidi kupunguza mipapai mingine hasa midume.

Mipapai yenye jinsi zote isizidi asilimia 10 – 20 ya miche yote iliyopo shambani, na midume ibaki mmoja katika kila majike 25.



Utunzaji



• Weka kilo 2 – 5 za samadi kwenye kila mpapai kwa mwaka ili kuongeza ukuaji na uzalishaji.

• Mabaki ya mimea yanaweza kuwekwa kama matandazo. Hii ni muhimu zaidi kipindi cha kiangazi ili kuzuia unyevu usipotee.

• Chunguza mipapai mara kwa mara ili kuangalia kama kuna magonjwa, ing’olewe na kuchomwa au kufukiwa chini endapo itabainika kuwa na maonjwa.

• Unaweza kunyunyiza dawa zisizo na madhara za kukinga au kukabiliana na magonjwa ya ukungu na virusi.



Kupogoa



• Kata matawi yote yatakayojitokeza pembeni ya mpapai. Hili lifanyike mapema kabla ya tawi kuwa kubwa.

• Ondoa mipapi yote ambayo hayakuchavushwa vizuri na ubakize yenye afya tu.



Palizi



• Mipapai inapopandwa tu inaweza kuwekewa matandazo kuizunguka ili kuzuia uoataji wa magugu.

• Magugu yang’olewe yakiwa machanga.

• Epuka kuchimbua sana wakati wa palizi kwa kuwa mizizi ya mipapai huwa juu juu.



Magonjwa



Zao la papai halina magonjwa mengi sana yanayoshambulia endapo litatunzwa vizuri. Hata hivyo kuna baadhi ya magonjwa ambayo yamezoeleka kwenye zao hili kama vile Ugonjwa wa madoa kwenye majani (Papaya spot) na Ugonjwa wa virusi unaojulikana kama Mozaic virus. Mimea yenye magonjwa inaweza kung’olewa na kufukiwa ili kudhibiti ueneaji kwenye mimea mingine.
Read More
  • 7:17 AM
  • Mbeya Info

Ufugaji na kilimo vinalipa

Nimeona mm pia nitoe testimonial kwa faida ya wajasiriamali wanaopenda kilimo na ufugaji.

Ndoto yangu imekuwa kutafuta ujasiriamali utakaoniwezesha kuachana na ajira at 40yrs.Baada ya kujaribu biashara mbalimbali nikagundua kuwa faida zilizopo kwenye kilimo na ufugaji ni kubwa mno especially kama una kamtaji ka kuanzia kapo.Nikaanza kutafuta mashamba.Nikapata kadhaa ila hili la Maseyu ndilo hasa linazaa matunda.kwa wale wanajua morogoro road, hicho kijiji kipo baada ya bwawani au km6 kabla ya mikese.Shamba lipo km1.5 toka barabarani.Nilinunua eka 100 mwaka 2011.

Immediately nikaanza kufyeka na kung'oa visiki.Nikalima eka10 za mahindi na alizeti mwishoni 2012.Nililima eka 2 za tikiti maji.mazao yanastawi si mchezo.masika ya 2013 nikalima eka 20 za alizeti na mahindi.pia nikaanzisha mradi wa nguruwe. Nilianza na nguruwe 8 jike na dume mmoja.sasa nina nguruwe kama 70 hv.Nilipata changamoto kidogo,nguruwe watatu walikufa.kwa changamoto hizo nimepata uzoefu mkubwa. Mambo mengi kama kuchoma chanjo na kutibu baadhi ya magonjwa naweza kufanya mwenyewe kwa maana madaktari nao ni changamoto.nategemea kuanza kuuza nguruwe wakubwa by April.wadogo nauza though soko lake sio kubwa sana.

Pamoja na upungufu wa mvuA mazao yangu ya vule yamekomaa.nna tikiti kama eka10 na mahindi kama eka25. Nextmonth nategemea kulima eka kama 70 hv.nataka kulima mahindi,alizeti,ufuta,mtama na maboga.vyote kwa biashara na chakula ya mifugo yangu.

Nataka niweze kuuza nguruwe 20 kila mwezi by this year. Mwaka jana nimevuna zaidi ya gunia 200 za mahindi na 150 za alizeti.fuso 2 za tikiti maji.Cha zaidi nimetoa ajira kwa vijana kazaa. Tatizo la maji shambani nimetatua last year kwa ku design bwawa na matank cheap.

Karibuni wajasiriamali,future ipo kwenye kilimo.
Read More
Home
Subscribe to: Posts (Atom)

Copyright © Mjasiriamali | Powered by Blogger